Wajita ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi hasa katika Mkoa wa Mara. Lugha yao ni Kijita.
Wajita wana muingiliano mkubwa na makabila kama Waha, Wahaya, Wanyankole, Wanyoro, Watoro, Wakerewe, Wahangaza, Wanyambo, Wazinza, Wakara, Wakabwa, Waruri, Wasweta, Wasimbiti, Wasubi, Wakwaya na kadhalika. Kulingana na historia yao wengi waweza kuitana wajomba. Bila kusahau Wajaluo ambao ni watani wao.
Wajita nao wana koo nyingi sana kama Abhajigabha, Abhegamba, Abhatata, Abhagaya, , Abhaanga, Abhalinga, Abhaila, Abhalaga, Abhatimba, Abhayango, Abhasyora, Abharungu, Abharamba, Abhakome, Abhagunda, Abhabhogo, Abhakima, Abhakumi na wengineo.
Wajita ni watu wachapakazi sana na wasiopenda dhihaka kwenye kazi, wenye msimamo sana na wenye kupenda utani na wapole, ila wakali sana wanapoonewa.
Tena Wajita wanapenda elimu na ndiyo maana tokea wamisionari walipofika eneo la Rusoli walijenga shule kisha kudahili wanafunzi wa kutosha.
Pia Wajita ni watu wenye ubunifu na uthubutu wa kufanya mambo yenye tija. Ni waasisi wa mabadiliko kifikra.